• JIJI LA MWANZA

    Hii ni moja ya sehemu muhimu katika jiji la Mwanza ambayo kwa namna moja ama nyingine imezidi kutoa muonekano mzuri hasa sehemmu za katikati ya jiji. ...

    SOMA ZAIDI
  • MT. AGOSTINO

    Moja ya vyuo vikuu vyenye heshima kubwa hapa nchini kipo jijini Mwanza na hii ni moja sura zenye muonekano wa kuvutia pindi unapofika chuoni hapo. ...

    SOMA ZAIDI
  • TANZANIA STARS

    Ni kipindi bora cha muziki wa dansi nchini kinachorushwa na Radio Free Africa, yes na huu ni ukurasa unaobeba kipindi hiki katika mtandao wa kijamii wa Facebook. ...

    SOMA ZAIDI

Sunday, March 30, 2014

alino piaza grand soliste


mimi ni mwanamuziki,si mwanasiasa

huku akijisifia kufuatia kualikwa na rais robert mugabe kufanya onyesho nchini zimbabwe katika harusi ya binti wa rais huyo,koffi olomide amesema uwezo wake mkubwa kimuziki ndo sababu ya kualikwa...mwamba huu kwa sasa unajivunia album ya abracadabra na singo ya mwaka 2013 yake na cyind iitwayo koffi central...

mashali kidedea

Thomas simba Mashali kulia ametwaa ubingwa wa ubingwa wa DUNIA IBF by unanimous decision dhidi ya kumchakaza Japhet Kaseba...hongera brother..

Saturday, March 29, 2014

BALLE DE MATCH ALBUM YA JB MPIANA SOOOOOOOOOOONNN

Taarifa rasmi kutoka ndani ya bendi ya WENGE BCBG chini ya mukulukulu JB MPIANA zinasema kwa uhakika kuwa albamu mpya ya BALLE DE MATCH ipo mbioni kutoka kwani kwa hivi sasa vinamaliziwa vitu vidogovidogo ambavyo hawajawa tayari kuvielezea..humo kuna baadhi ya vibao jb amemshirikisha PAPA WEMBA...album hii inakuja kuchukua nafasi ya ile ya zamani ya SOYONS SERIEUX iliyotisha na mitindo kama mpunda,telecomanndre ....kila la heri BINADAMU..

JKT MBWENI KUIBUKA KIDEDEA LEO?

Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya netiboli ya klabu bingwa Afrika Mashariki JKT MBWENI leo inatarajiwa kuibuka mabingwa wa michuano hiyo baada ya kuifunga Prisons ya Uganda mabao 35-33.Timu hiyo itacheza na mabingwa watetezi NIC kutoka Uganda ambao waliibabajua Moict kutoka Kenya kwa mabao 49-32....KILA LA HERI JKT MBWENI..

VIWANJA BADO TATIZO SOKA LA VIJANA

LICHA ya kuwa na vipaji lukuki,bado tatizo la maeneo sahihi ya kucheza mpira kwa watoto ni tatizo.Vijana wengi wanapenda sana kucheza mpira na wana ndoto za kufika mbali hata hivyo ukosefu wa viwanja bado ni kikwazo kikubwa kwa vijana hao kufikia kiwango cha kuisaidia timu ya taifa.Watoto wengi wamekuwa wakilazimika kufunga safari ndefu ili kupata viwanja vizuri vya kuonyesha vipaji vyao.Mfano wa ukosefu wa viwanja ni jijini Mwanza ambapo blogi hii imeshuhudia michuano ya vijana chini ya miaka 17 ikichezwa katika viwanja vibovu kabisa ambavyo huhatarisha usalama wa afya za wachezaji vijana pindi wanapoumia..Makocha wa East Boys Amiri Yasini na Joki Dominic wa TSC wamebainisha hayo jijini Mwanza katika michuano hiyo..

NANI ZAIDI KASEBA NA MASHALI?LEO NDO LEO PTA..

Bondia Japhet Kaseba akiinua mikono juu wakati wa kupima uzito kwa ajili ya pambano lake la ubingwa wa Taifa, uzito wa Middle dhidi ya Thomas Mashali kushoto litakalofanyika Ukumbi wa PTA, Sabasaba, Dar es Salaam LEO..

BAVICHA YAILAUMU CCM


BARAZA la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), limelaani vikali njama walizodai kufanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutengua kanuni ili waweze kuliteka Bunge Maalumu la Katiba kwa kupitisha maoni yao badala ya maoni ya wananchi yaliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Katibu wa BAVICHA, Bw. Deogratias Munishi, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa, kutengua kanuni hizo ni kuwakosea adabu wananchi wenye kiu ya kupata Katiba Mpya.
Alisema mfumo wa muundo wa Serikali uliopendekezwa katika Rasimu ya Pili (Serikali tatu), ndio inayofaa kudumisha umoja na mshikamano wa Watanzania tofauti na mfumo wa Serikali mbili unaopendekezwa na CCM.
 

Alisema Serikali ya CCM inaandika Katiba Mpya kwa shinikizo la wananchi hivyo lazima watambue kuwa, wananchi walioshinikiza ndio hao ambao watasimama kidete kupata katiba wanayoitaka ambapo vijana wote lazima watambue kuwa, chama tawala hakina mpango wa kuona nchi inapata Katiba Mpya.
 

"BAVICHA inalaani vikali njama zinazofanywa na CCM kutaka kuharamisha kanuni ili kuliteka Bunge hili, mfumo wa Serikali mbili unaopendekezwa na CCM umepandikiza chuki miongoni mwa wananchi waishio pande mbili za Muungano," alisema.
 

Bw. Munishi aliongeza kuwa, hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa hivi karibuni katika Bunge hilo, imeleta mgawanyiko miongoni mwa wajumbe badala ya kuleta maridhiano kwenye mambo ambayo yatakuwa magumu kuamuliwa na wajumbe.
 

Aliwataka wananchi kukataa kuburuzwa au kushuhudia Katiba mbovu inapatikana na kuivumilia CCM pamoja na wapambe wake ambao wameamua kuhujumu maoni yaliyomo kwenye Rasimu ya Pili kupitia Bunge hilo.


Tuesday, March 25, 2014

UVUVI HARAMU KUFIKA KIKOMO..

Wadau wa sekta ya uvuvi kanda ya ziwa wamekutana hapo jana jijini Mwanza kujadili namna ya kudhibiti matendo yote ya uvuvi usiofuata utaratibu....wamesema kwa kauli moja aina hiyo ya uvuvi imepata muarobaini wa uhakika....wamesema sheria kali zimewekwa ikiwemo ile ya vifungo,faini ama vyote kwa pamoja...wamebainisha kuwa chanzo kikubwa cha tatizo hilo ni siasa ambapo wanasiasa wamekuwa wakiwahamasisha wapiga kura wao kutoacha aina hiyo ya uvuvi..madhara ya aina hii ya uvuvi hasa matumizi ya nyavu zisizo na viwango,matumizi ya sumu na mabomu ni pamoja na uchafuzi wa ziwa,kuua mazalia ya samaki na viumbe vingine vya majini,kusababisha magonjwa hasa ya matumbo kwa binadamu,vifo n.k....mkutano huo wa wadau umehisaniwa na TAFU,TAFIR...

EPL KUCHANJA MBUGA LEO...

Ligi kuu ya Uingereza inaendelea leo,Emirates,Old Trafford na St James burg....arsenal baada ya kuburuzwa mabao 6 leo wanajiwinda kwa Swansea,Manchester United watawathibitishia mashabiki wao kuwa shetani hazeeki mbele ya miamba ya Manchezter City huku Newcastle wakitoana jasho na Everton....kura yako unaitupa wapi?

AJALI...

Watu 107 wamefariki dunia,katika ajali ya kuzama kwa boti,katika mpaka wa Uganda na Kongo..watu 41 kati ya 250 waliokuwemo katika boti hiyo wakati ikizama wameokolewa...

POLENI WANA MARA..

Mkuu wa mkoa wa Mara John Gabriel Tupa amefariki dunia ghafla hii leo asubuhi majira ya saa 4:30 mara baada ya kupatwa ghafla na shiikizo la damu akiwa wilayani Tarime mkoani humo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizo tufukia toka chanzo chetu kikuu zinasema kuwa marehemu John Tupa amefariki mara baada ya kuanguka ghafla akiwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime Jackson Msome wakati alipokwenda ofisini hapo kwa ajili ya mazungumzo pamoja na kushauriana masuala mbalimbali ya utekelezaji.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa Baada ya kuanguka Tupa alikimbizwa hospitali ya wilaya ya Tarime ili kupatiwa matibabu lakini kwa bahati mbaya madaktari waligundua kuwa tayari amefariki dunia. 

Mwili wa marehemu tayari umesafirishwa kutoka Tarime kuelekea Musoma mjini kwa ajili ya kuhifadhiwa ukisubiri taratibu nyingine na maelekezo ya kiserikali.

Sunday, March 23, 2014

mgogoro wa tanzania na malawi utamalizwa kwa kuweka mipaka ziwa nyasa...

joaquim chissano,rais wa zamani msumbiji,mkuu wa chissano foundation na mkuu wa jopo la marais watatu wastaafu wanaotafuta mbinu za kuumaliza mzozo baina ya nchi hizo,kasema hili litakuwa suluhisho la kudumu..ameyasema haya katika kikao cha viongozi hao..kikao kingine kitafanyika mwezi may baada ya uchaguzi nchini malawi..

rekodi mpya jana classico


This El Clasico was open..
with plenty of goals...
controversy, of course there was controversy -- three penalties and a red card worth -- 
and of course about one man - a gifted little Argentine - coming to the fore like only he can under immense pressure to put his team right back in the La Liga title race.
Lionel Messi not only go top of the charts in El Clasico goalscorers list, but also to give Barcelona a thrilling come-from-behind victory over Real Madrid.
Ramos' 13th sending off in 14 El Clasico's, and the 19th of his career...
Messi, of course he didn't, despite the Real players seething behind him, was ice-cool, slotting home -- his 21st El Clasico goal, a new record going past Alfredo Di Stefano's mark of 18, and 236th La Liga goal to go second on the all-time list -- to give Barcelona a famous victory.
4-3...was the result...
source..d.vikraman@ibtimes.co.in

Saturday, March 22, 2014

JAMANI WATU WAMETOKA MBALI,MUONE DEKULA VUMBI KAHANGA AKIWA NA ORCHESTRA MARQUIZ 1987...

Hapa ni SUPER MINI BAR..hahahahaaaaaa enzi hizo kila jumapili mchana..jamani..msiomjua huyu mzee ni mkali wa solo....mayanga weeeeee..

HALI ILIVYOKUWA HAPO JANA BUNGENI..


HOTUBA YA JK UZINDUZI BUNGE LA KATIBA YAWAKOSHA WATANZANIA...

Hotuba ya rais Jakaya Mrisho Kikwete hapo jana akizindua rasmi bunge la katiba umepokelewa kwa hisia tofauti huku asilimia kubwa ya watanzania wakiipongeza kutokana na kuonekana kulenga kulinda maslahi ya taifa.Blogi hii hapo jana wakati hotuba ya rais ikiendelea kupitia vyombo mbalimbali vya habari ilipitia mitaa kadhaa na kukuta kila sehemu wananchi wakifuatilia kwa umakini mkubwa.Mambo yanayopongezwa ni kauli ya raisi kuwataka watu kutoa mawazo yao binafsi pasipo kushinikizwa,kuzingatia maslahi ya taifa kwanza na kuepusha migogoro wakati wa mchakato mzima.Hata hivyo waliopinga hotuba hiyo wamesema imejikita katika maoni binafsi ya raisi pia ya chama chake.Bunge hilo la katiba lipo chini ya uenyekiti wa Samuel Sitta huku uwakilishi wa wananchi ukitokana na wabunge,wanaharakati,wadau wa maendeleo,wasomi na wananchi wa kawaida.