VIWANJA BADO TATIZO SOKA LA VIJANA

Posted by Bernard James on 1:57 AM with No comments
LICHA ya kuwa na vipaji lukuki,bado tatizo la maeneo sahihi ya kucheza mpira kwa watoto ni tatizo.Vijana wengi wanapenda sana kucheza mpira na wana ndoto za kufika mbali hata hivyo ukosefu wa viwanja bado ni kikwazo kikubwa kwa vijana hao kufikia kiwango cha kuisaidia timu ya taifa.Watoto wengi wamekuwa wakilazimika kufunga safari ndefu ili kupata viwanja vizuri vya kuonyesha vipaji vyao.Mfano wa ukosefu wa viwanja ni jijini Mwanza ambapo blogi hii imeshuhudia michuano ya vijana chini ya miaka 17 ikichezwa katika viwanja vibovu kabisa ambavyo huhatarisha usalama wa afya za wachezaji vijana pindi wanapoumia..Makocha wa East Boys Amiri Yasini na Joki Dominic wa TSC wamebainisha hayo jijini Mwanza katika michuano hiyo..