• JIJI LA MWANZA

    Hii ni moja ya sehemu muhimu katika jiji la Mwanza ambayo kwa namna moja ama nyingine imezidi kutoa muonekano mzuri hasa sehemmu za katikati ya jiji. ...

    SOMA ZAIDI
  • MT. AGOSTINO

    Moja ya vyuo vikuu vyenye heshima kubwa hapa nchini kipo jijini Mwanza na hii ni moja sura zenye muonekano wa kuvutia pindi unapofika chuoni hapo. ...

    SOMA ZAIDI
  • TANZANIA STARS

    Ni kipindi bora cha muziki wa dansi nchini kinachorushwa na Radio Free Africa, yes na huu ni ukurasa unaobeba kipindi hiki katika mtandao wa kijamii wa Facebook. ...

    SOMA ZAIDI

Wednesday, January 8, 2014

NBS YATOA CHANGAMOTO KWA WATANZANIA

Viwanda - 2
 Mkurugenzi wa Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Morrice Oyuke ametoa wito huo wakati akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam kutoa taarifa ya fahirisi za uzalishaji wa bidhaa za viwandani hadi kufikia mwaka 2012 zilizowekwa katika makundi mbalimbali kwa kufuata mwongozo wa Umoja wa Mataifa.



Wito umetolewa kwa watanzania kujitokeza kwa wingi katika kuanzisha na kumiliki viwanda vitakavyozalisha bidhaa mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kuongeza ajira, kukuza pato la taifa na kupunguza hali iliyopo ya uagizaji wa bidhaa mbalimbali toka nje ya nchi.
Mkurugenzi wa Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Morrice Oyuke ametoa wito huo wakati akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam kutoa taarifa ya fahirisi za uzalishaji wa bidhaa za viwandani hadi kufikia mwaka 2012 zilizowekwa katika makundi mbalimbali kwa kufuata mwongozo wa Umoja wa Mataifa.
Amesema kuwa ongezeko la viwanda nchini licha ya kuongeza ajira kitakwimu lina mchango mkubwa katika kusaidia kupima fahirisi za uzalishaji wa bidhaa za viwandani na kuongeza  kuwa uzalishaji wa bidhaa za viwandani hupima mabadiliko ya kiasi cha bidhaa zilizozalishwa na wazalishaji mbalimbali ambao kwa wastani wamejiajiri kuanzia wafanyakazi 50 na kuendelea.
Amefafanua kuwa Tanzania katika kipindi cha mwaka 2006 hadi 2012 imekua na kiwango cha juu cha mabadiliko ya fahirisi ya bei ya uzalishaji wa bidhaa za viwandani kwa jumla ya asilimia 10.8 ikilinganishwa  na asilimia 2.1 za mwaka 2011.
Ameongeza kuwa fahirisi za uzalishaji wa bidhaa za viwandani kwa mwaka 2012 zimeongezeka na kufikia 328 ikilinganishwa na 296 za mwaka 2011 na kuongeza kuwa ongezeko hilo limechangiwa na uzalishaji wa vinywaji na tumbaku kwa asilimia 16.8%, Viwanda vya chuma 14.6% na ongezeko na bidhaa za nguo na ngozi kwa asilimia -17.7%.
Bw. Oyuke ameyataja makundi mengine yatokanayo na bidhaa za viwandani kuwa ni pamoja na Mbao na bidhaa za mbao 0.3%, Karatasi na bidhaa za karatasi 5.0%, Kemikali, Petroli na bidhaa za Plastiki -7.9%, Bidhaa za udongo, vioo na bidhaa zisizo za metaliki 7.5% na bidhaa zitokanazo na chuma 11.0% .
Naye mtafiti na mtaalam wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof. Haji Semboje akizungumza wakati wa mkutano huo amesema kuwa mfumo wa uzalishaji na biashara nchini unatokana na uwepo wa bidhaa za Kilimo na zile zisizo kuwa za kilimo na kuongeza kuwa juhudi kubwa zinahitajika katika kuwahamasisha Watanzania kumiliki viwanda vidogo, vya kati na vile vikubwa.
“Bado tunakabiliwa na changamoto ya umiliki wa viwanda hapa nchini kwa sababu viwanda vingi vikubwa vinamilikiwa na wageni, watanzania walio wengi wanamiliki viwanda vidogo vidogo” amesema Prof. Semboje.
Ameongeza kuwa hivi sasa kuna ongezeko kubwa la bidhaa mbalimbali zikiwemo nguo kutoka nje ya nchi jambo ambalo linaathiri uchumi wa ndani na kusisitiza kuwa kuwa juhudi zinahitajika katika udhibiti wa bidhaa zisizokidhi viwango na ambazo hazina chapa ya eneo zilikotengenezwa ambazo zinapatikana katika masoko ya Tanzania.
Prof. Semboje ameeleza kuwa kutokana na kuongezeka kwa uwezo wa watanzania kununua, kuagiza na kufanya biashara nje ya nchi ipo haja ya watanzania hao  na serikali kwa ujumla kupitia mamlaka husika za uwezeshaji wananchi kiuchumi kuangalia uwezekano wa kuwajenga uwezo wa kununua mitambo inayozalisha bidhaa hizo  na kuileta ndani ya nchini kwa lengo la kuongeza pato la taifa na kuwawezesha wananchi kiuchumi.
“ Ninapenda kutoa wito kwa Taasisi za Uwekezaji nchini kutoa kipaumbele kwa Watanzania katika suala la uwekezaji wa ndani pia kutoa elimu zaidi kwa watanzania katika uzalishaji wa kisasa kwa sababu tayari serikali imeshaweka mipango mizuri ya kuwaendeleza watanzania, changamoto tuliyonayo ni kuitafsiri mipango na sera zilizopo kwa manufaa ya nchi”

RAIS – AKUTANA NA WAZIRI WA NISHATI NA MIGODI WA ALGERIA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Mhe. Youcef Yousif aliyemtembelea Ikulu Dar es salaam Leo Januari 7, 2014 algeria2 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya Pamoja na Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Youcef Yousif pamoja na ujumbe wake, pamoja na Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania Profesa Sospter Muhongo Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe Steven Masele na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini  Mhe E. maswi  ugemi huo ulipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 7, 2014. algeria3 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Mhe. Youcef Yousif aliyemtembelea Ikulu Dar es salaam leo Januari 7, 2014 algeria4 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya Pamoja na Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Youcef Yousif pamoja na ujumbe wake, pamoja na Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania Profesa Sospter Muhongo Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe Steven Masele na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini  Mhe E. maswi  ugemi huo ulipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 7, 2014. algeria5 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Mhe. Youcef Yousif aliyemtembelea Ikulu Dar es salaam leo Januari7, 2014.
……………………………………………………………………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Januari 7, 2014, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nishati na  Migodi  wa Algeria Mheshimiwa  Youcef Yousfi ambaye yuko katika ziara ya siku sita nchini.
Katika ziara hii, Mheshimiwa Yousfi na ujumbe wake unaojumuisha viongozi wa mashirika ya umma, wanatarajia kutembelea kituo cha umeme cha Gridi ya Taifa cha Ubungo mjini Dar es Salaam, ujenzi wa bomba la gesi katika eneo la Vikindu na Mkuranga mkoani Pwani, machimbo ya Mererani  na Minjingu mkoani Manyara.
Rais Kikwete ameeleza kufurahishwa kwake na ziara hiyo, akisisitiza kwamba Tanzania na Algeria zimekuwa marafiki na washirikia wa karibu wa siku nyingi katika masuala ya siasa na uchumi, kufuatia  misingi imara iliyowekwa na waasisi wa nchi hizo – Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mheshimiwa Ahmed Ben Bella,
Rais amebainisha kwamba ushirikiano wa nchi hizi mbili  ni muhimu sana sio tu katika kuendeleza uhusiano wao wa  muda mrefu, bali pia katika  uwekezaji na utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi pamoja na uendelezaji wa rasilimali watu.

JUMUIYA YA DARAJA FONDATION YAJITAMBULISHA ZANZIBAR.

01 

Mkurugenzi mtendaji wa Daraja Fonndation Bi. Arsheen Dhalla yenye Makao Makuu yake Canada akiitambulisha Jumuiya yao inayojishuhulisha na sekta ya Afya, Elimu na Watoto mayatima katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Amore Mio Mjini Zanzibar.

MAASKOFU WAMTEMBELEA RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI

DCIM100MEDIA Mratibu wa Dua Maalum ya kuiyombea Zanzibar kwa ajili ya mwaka mpya wa  2014  Allen Mbaga akizungumza na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi walipomtembelea na kumuombea nyumbani kwake Maisara ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. DCIM100MEDIA 
Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi akipokea zawadi kutoka kwa binti wa Mratibu wa Dua maalum ya kuiombea Zanzibar, Clare Allen Mbaga walipomtembelea na kumuombea nyumbani kwake Maisara ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
DCIM100MEDIA 
Picha ya pamoja ya Kamati maalum ya kuiyombea Zanzibar kwa ajili ya mwaka mpya 2014 na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi ilipomtembelea nyumbani kwake Maisara ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka 50 ya Mpinduzi ya Zanzibar.
(Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar).

MKUU WA MKOA AMFUKUZA MKANDARASI KATIKA MKOA WAKE

IMG_0999 
Mkuu wa mkoa wa Rukwa injinia Stella Manyanya (kulia) akizungumza wakati akikagua jengo hilo la bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Kasanga wilayani Kalambo. Pembeni yake ni Mhandisi wa ujenzi wa wilaya ya Kalambo Issa Liyanga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Philbert Ngaponda. 

PICHA NA RAMADHANI JUMA-AFISA HABARI WILAYA YA KALAMBO 

Mkuu wa mkoa wa Rukwa injinia Stella Manyanya akizungumza wakati akikagua jengo hilo la bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Kasanga wilayani Kalambo. Kulia ni mhandisi wa ujenzi wa wilaya ya Sumbawanga Vijijini ndugu Mtapima na katikati ni Mhandisi wa ujenzi wa wilaya ya Kalambo Issa Liyanga.PICHA NA RAMADHANI JUMA-AFISA HABARI WILAYA YA KALAMBO  IMG_0996 
Mhandisi wa ujenzi wa wilaya ya Kalambo Issa Liyanga akimuonesha kitu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa injinia Stella Manyanya alipokagua jengo la bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Kasanga wilayani Kalambo.

ZITTO KIDEDEA, AIBWAGA CHADEMA MAHAKAMA KUU LEO

 HONGERA: Wakili wa CHADEMA Tundu Lisu (kulia) akilazimika kumpongeza aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe baada ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, John Mkamwa, kuridhia zuio la Zitto asijadiliwe na ngazi yoyote ya maamuzi ya Chadema, hadi kesi ya msingi aliyofungua dhidi ya chama hicho itakapomalizika. Jaji huyo amekubali kesi ya msingi iungurume na itaanza kusikilizwa Februari 13, mwaka huu. (PICHA NA THENKOROMOBLOG)
 Zitto akitoka kwa msaada wa mabaunsa wake katika chumba cha mahakama kuu baada ya uamuzi huo wa  Mahakama kuu leo jioni.
Tundu Lisu na wapambe wake wakionekana kutoka kwa aibu Mahakamani baada ya kubwagwa

 Tundulisu aklizungumza na waandishi nje ya mahakama
 Wakili wa Zitto akizungumza na waandishi nje ya mahakama kuu
 Wafuasi wa Chadema wanaomuunga mkono Zitto wakishangilia abaada ya ushindi wa kiongozi huyo
Wafuasi wa Chadema wanaomuunga mkono Zitto wakiwa wamekaa chini kutii amri ya polisi baada ya matokeo ya kesi kutangazwa upende wao ukiwa aumeibuka kidedea

 Wafuasi wa Chadema wanaounga mkono uongozi wa chama hicho kutaka Zitto atimuliwe uanachama, wakiwa wameduwaa nje ya mahakama baada ya uamuzi wa Jaji, John