RAIS – AKUTANA NA WAZIRI WA NISHATI NA MIGODI WA ALGERIA
Posted by Bernard James on 4:42 AM with No comments
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri wa Nishati na Migodi wa
Algeria Mhe. Youcef Yousif aliyemtembelea Ikulu Dar es salaam Leo Januari 7, 2014

Rais
Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya Pamoja na Waziri wa Nishati na
Migodi wa Algeria Youcef Yousif pamoja na ujumbe wake, pamoja na Waziri
wa Nishati na Madini wa Tanzania Profesa Sospter Muhongo Naibu Waziri wa
Nishati na Madini Mhe Steven Masele na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini Mhe E. maswi ugemi huo ulipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 7, 2014.

Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Nishati na
Migodi wa Algeria Mhe. Youcef Yousif aliyemtembelea Ikulu Dar es salaam
leo Januari 7, 2014

Rais
Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya Pamoja na Waziri wa Nishati na
Migodi wa Algeria Youcef Yousif pamoja na ujumbe wake, pamoja na Waziri
wa Nishati na Madini wa Tanzania Profesa Sospter Muhongo Naibu Waziri wa
Nishati na Madini Mhe Steven Masele na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini Mhe E. maswi ugemi huo ulipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 7, 2014.

Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Waziri wa Nishati na Migodi wa
Algeria Mhe. Youcef Yousif aliyemtembelea Ikulu Dar es salaam leo
Januari7, 2014.
……………………………………………………………………….
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Jumanne, Januari 7, 2014, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri
wa Nishati na Migodi wa Algeria Mheshimiwa Youcef Yousfi ambaye yuko
katika ziara ya siku sita nchini.
Katika
ziara hii, Mheshimiwa Yousfi na ujumbe wake unaojumuisha viongozi wa
mashirika ya umma, wanatarajia kutembelea kituo cha umeme cha Gridi ya
Taifa cha Ubungo mjini Dar es Salaam, ujenzi wa bomba la gesi katika
eneo la Vikindu na Mkuranga mkoani Pwani, machimbo ya Mererani na
Minjingu mkoani Manyara.
Rais
Kikwete ameeleza kufurahishwa kwake na ziara hiyo, akisisitiza kwamba
Tanzania na Algeria zimekuwa marafiki na washirikia wa karibu wa siku
nyingi katika masuala ya siasa na uchumi, kufuatia misingi imara
iliyowekwa na waasisi wa nchi hizo – Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na
Mheshimiwa Ahmed Ben Bella,
Rais
amebainisha kwamba ushirikiano wa nchi hizi mbili ni muhimu sana sio
tu katika kuendeleza uhusiano wao wa muda mrefu, bali pia katika
uwekezaji na utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi pamoja na
uendelezaji wa rasilimali watu.
0 comments:
Post a Comment