HOTUBA YA JK UZINDUZI BUNGE LA KATIBA YAWAKOSHA WATANZANIA...

Posted by Bernard James on 1:43 AM with 2 comments
Hotuba ya rais Jakaya Mrisho Kikwete hapo jana akizindua rasmi bunge la katiba umepokelewa kwa hisia tofauti huku asilimia kubwa ya watanzania wakiipongeza kutokana na kuonekana kulenga kulinda maslahi ya taifa.Blogi hii hapo jana wakati hotuba ya rais ikiendelea kupitia vyombo mbalimbali vya habari ilipitia mitaa kadhaa na kukuta kila sehemu wananchi wakifuatilia kwa umakini mkubwa.Mambo yanayopongezwa ni kauli ya raisi kuwataka watu kutoa mawazo yao binafsi pasipo kushinikizwa,kuzingatia maslahi ya taifa kwanza na kuepusha migogoro wakati wa mchakato mzima.Hata hivyo waliopinga hotuba hiyo wamesema imejikita katika maoni binafsi ya raisi pia ya chama chake.Bunge hilo la katiba lipo chini ya uenyekiti wa Samuel Sitta huku uwakilishi wa wananchi ukitokana na wabunge,wanaharakati,wadau wa maendeleo,wasomi na wananchi wa kawaida.